Msichana huyu Aisha Nabukeera alichomwa na mama yake wa kambo mnamo mwaka 2006. Habari hii iligonga sana vichwa vya habari vya Afrika Mashariki. Mfanyabiashara mwenye mafaniko Frank Gashumba alimchukua na Kumfanya Mtoto wake na kumsomesha. Sasa hivi amefaulu mtihani wake wa kidato cha sita na anategemea kujiunga na Elimu ya Chuo kikuu na ndoto zake ni kusomea sheria. Chanzo:JF |
↧
Aliyechomwa afauru
↧
AZAM YAMTIMUA OMOG

Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14.
Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidiI wake Ibrahim Shikanda.
Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidiI wake Ibrahim Shikanda.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya George Best Nsimbe
↧
↧
TANZANIA INAPOTEZA MABILIONI KWA RUSHWA
Tanzania inapoteza mabilioni ya fedha kwa rushwa na udanganyifu unaofanywa na watumishi wa TRA
.jpg)
Serikali imekiri kuwa Tanzania inaendelea kupoteza mabilioni ya fedha za umma kutokana na rushwa na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa mamlaka ya mapato (TRA) kwa kuvusha mizigo mikubwa bila kulipa kodi kwa kudanganya kuwa ni mali ghafi huku mingine ikidaiwa kupelekwa nje ya nchi na kuuzwa njiani hali inayo wafanya wananchi kukosa imani na taasisi za serikali.
Waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora GEORGE MKUCHIKA ametoa kauli hiyo jiji Arusha alipokuwa anazungumza na watendaji wa mamlaka ya mapato takukuru na viongozi wa dini katika kikao cha mpango mkakati wa TRA kupambana na rushwa kwa kuwashirikisha wadau na kuongeza kuwa watanzania wamechoka kusikia upotevu wa mabilioni ya fedha za umma kwa ajili ya kunyakuliwa na watu wachache.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya amani ya viongozi wa dini SHEKH ALHAD MUSA amesema TRA imekuwa ikilalamikiwa sana na wananchi kuhusu kushamiri kwa rushwa hivyo kuna muhimu wa viongozi wa dini kutoa semina za neno la mungu kwa watumisi huku msaidizi wa askofu wa kanisa la KKKT Diosisi ya mashariki na pwani GEORGE FUPE akidai kabla kutengeneza mipango mkakati inapaswa kila mmoja ajitathimini kama inatosha kuwepo katika nafasi yake.
Chanzo.itv
Chanzo.itv
Kamishina mkuu wa mamlaka ya mapato nchini TRA, RISHED BADE amesema TRA ni taasisi iliyopo katika mazingira hatarishi kwa vishawishi vya rushwa lakini bado mikakati inafanyika kuondoa hali hiyo na sasa wameanza kushirikisha wadau katika kuianda mikakati mikakati hiyo.
↧
Watu saba wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukata kiganja cha Albino
.jpg)
Jeshi la polisi mkoani rukwa linawashikilia watu saba hadi sasa, kwa tuhuma za kuhusika na kitendo cha kikatili cha kukata kiganja cha mkono wa kulia, cha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Baraka Cosmas Lusambo mwenye umri wa miaka sita, katika kitongoji cha kikonde kata ya kipeta wilaya ya sumbawanga vijijini, ambapo pia katika tukio hilo wamemjeruhi mtoto huyo mkono wa kushoto.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa rukwa kamishna msaidizi wa polisi Leons Rwegasira, amesema wamefanikiwa kuwakamata watu hao kufuatia msako mkali, mara tu baada ya kutokea tukio hilo kwenye kitongoji hicho cha kikonde, ambacho kinakuwa na wakazi wakati wa msimu wa kilimo na kiangazi watu wanahama tena, katika familia yenye watoto wengine watatu wenye ulemavu wa ngozi.
ACP.Rwegasira pia amesema kwenye msako huo mkali, wamefanikiwa kuwakamata watu wanane wanaojihusisha na uganga wa jadi na upigaji wa ramli chonganishi, ambacho ni chanzo kikubwa cha kusababisha vifo na kujeruhiwa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa imani za kishirikina.
Mtoto baraka na mama yake mzazi wamelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya jijini mbeya, wakitibiwa majeraha waliyoyapata wakati wa purukushani za kumshambuliwa mtoto huyo.
↧
Imetosha

↧
↧
Kijiji cha Mtimbwilimbi
↧
MH.LOWASA NA MAANDAMANO YA KUPINGA MAUAJI ALBINO-TEMEKE
↧
SERIKALI - HAKUNA MTANZANIA ALIYEKUFA AFRIKA KUSINI
Serikali imesema hakuna mtanzania aliyeuawa katika matukio ya mauji ya chuki za kibaguzi (ZENOPHOBIA) yanayofanywa na raia wa Afrika Kusini dhidi ya wageni na tayari imeanza mpango wa kuwarudisha nyumbani watanzania 21 kati ya 23 waliohifadhiwa katika kambi kwenye mjini DURBUN nchni humo kwa ajili ya usalama.
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe amesema vifo vya watanzania watatu vilivyotokea nchni humo havina mahusiano na mauaji hayo ZENOPHOBIA na kusisitiza serikali ya afrika kusini imeanza kuchukua hatua na tayari watu wawatu waliohusika na kifo cha rais wa msumbiji wamekamatwa.
Akizungumzia idadi ya watanzania waliohifadhiwa kwenye
Kambi katika mji wa DURBUN,Mhe Membe amesema takribani watanzania 23 wamehifadhiwa katika kambi ya isipingo iliyo na zaidi ya raia wa kigeni elfu tatu ambao wako chini ya ulinzi wa serikali ya afrika kusini na kusisitiza serikali imeanza utaratibu wa kuwarudisha nyumbani watanzania 21 kati yao.
Akielezea msimamo wa tanzania kufuatia mauaji hayo ya ZENOPHOBIA yanayoendelea nchni afrika kusini,Mhe. Membe amesema serikali inaunga na jumuiya ya nchi za SADC kulaani vitendo vya mauaji yanayoendelea nchni humo ambapo watu 8 wamekwisha uawa kikatili na kuita serikali ya afrika kusini kuzuia mauaji hayo haraka iwezekanavyo.
Aidha amesema serikali ya Tanzania haitakuwa na tatizo la watanzania kurudi nchni humo baada ya mauaji kudhibitiwa na kwa upande wa wafanyabishara walisajiliwa kihalali na kupoteza mali zao, serikali itawasiliana na wanasheria wake ili kuona namna ya kutafuta namna ya nchi hiyo kuwafidia hasara waliyoipata.
↧
Matengenezo barabara ya Msimbazi
↧
↧
BARABARA BADO JANGA
↧
KOTA ZA TEMEKE MWISHO YAGEUKA GEREJI BUBU
↧
NASH MC NA MIAKA 16 YA JUMA NATURE
Hiki ndio alichokisema msanii wa hiphop nchini Nash Mc katika kuelekea miaka 16 ya Juma Nature
Nawapongeza E.FM 93.7 kwa kuandaa Tamasha la miaka 16 katika game ya Sir Juma Nature, hakuna asietambua mchango wa Juma katika kuifikisha sanaa yetu hapa ilipo ukiacha nyota aliyokua nayo ya kupendwa na watanzania wengi, Ni jambo zuri sana na la kuigwa na Media zingine nchini, maana wengi husubiri wasanii wafe watumie mwanya huo kujipatia kipato kwa kuandaa matamasha ya kumkumbuka Hayati huyo,kama ilivyokua kwa Hayati Albert Mangwear, E.FM wamefanya kitu ambacho Alipaswa kufanyiwa Sir Juma Nature muda tu lakini si haba natumai litakua tamasha zuri na kubwa ntajitahidi niwepo siku hiyo kwa kua itakua nyumbani Temeke basi mzukaaaa.
16 Ya Sir Juma Nature katika Game.
↧
NATURE ADHIHIRISHA UKUBWA WAKE
Nature akiweka maiki vizuri ili akamue ipasavyo.
Profesa J akiwapa mashabiki kitu walichotaka.
SHOO ya kutimiza kutimiza miaka 16 katika muziki kwa msanii Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’ na kituo cha Utangazaji cha EFM kutimiza mwaka mmoja iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Burudani wa Taifa wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, lilikuwa moto wa kuotea mbali.Katika onyesho hilo Nature, mbali ya kutoa burudani ya nguvu, alipigwa tafu na Snura, Profesa J. Makomandoo, Shetta na Msaga Sumu.
↧
↧
barabara ya likwati wailes yakamilika
↧
UTAMBULISHO WA MGOMBEA WA URAISI WA CCM. DR. MAGUFULI VIWANJA VYA ZAKHEIM
↧
NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA INTERN.AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN ,JUMAMOSI 25 JULAI 2015
FFU-Ughaibuni Jino kwa Jino na Washabiki wa Tubingen Jumamosi 25,07.2017
Tübingen,Ujerumani
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani,inatarajiwa kutingisha jukwaa la
maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni barani ulaya 6th International African Festival in Tübingen, Ujerumani, bendi hiyo maarufu inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja itapanda jukwaani siku ya Jumamosi 27 Julai 2015 majira saa 2.00 Usiku katika
uwanja wa Festplatz,Europa str,mjini Tübingen ,uliopo Ujerumani ya Kusini.
Kikosi kazi hiko cha Ngoma Africa Band ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki au FFU,chenye utajiri wa wanamuziki vijana waliojaa vipaji, bendi inasadikiwa kuwanasa
washabiki kila kona duniani kutokana na mdundo wake"Bongo Dansi" made in Uswahilini. bendi hiyo kwa sasa inatamba na CD mpya ya " La Mgambo" yenye nyimbo mbili za kumuaga rais JK.
Usikose kuwasikiliza at www.reverbnation.com/
↧
UANDIKISHAJI WAPIGA KURA TEMEKE
↧
↧
HII IMEKUAJEEEE! !!
HII INAKUWAJE..................
Hiki ninaweza kuita ni kioja katika moja ya vioja vingi vilivyotokea katika mwaka huu.. hakika inasikitisha sana katika zoezi linaloendelea la uandikishaji la wapiga kura kwa mfumo wa Kielektroniki (Biometric Voters Registration) kuna vitu vya aibu vinafanyika vinavyodhalilisha nchi kuonekana kama kwamba ina uhaba mkubwa wa watu wenye maarifa ya kuweza kutenda kazi.
kwa mfano; uchukuaji na uwekaji wa picha (pass port) tazama picha iliyowekwa katika hicho kitambulisho hauhitaji kuwa na elimu yoyote kujua hiyo picha haiko sawa na ukichukulia kwamba vitu vya msingi katika kitambulisho ni maelezo (Particulars), saini na picha (Passport size) sasa hiyo picha hapo ni passport, post card au ni kitu gani? Na hiki kitambulisho kinawakilisha vitambulisho vingi (si vyote) vilivyotolewa katika hili zoezi kwa mtindo huo.Ukiachilia huo utendaji na hata muonekano wa nyuma ya picha (background) ni mbovu haupendezi hata kidogo
Mfano wa umuhimu wa picha angalia pale unapohitaji Hati ya kusafiria (Passport) unapopewa vigezo ya picha wanayohitaji au hivi ni vigezo tumepewa na wazungu kwa kuwa matumizi ya Pass port ni ulimwenguni kote (worl wide) na tusipofuata Raia wetu hawataweza kusafiri popote na hiki kitambulisho cha kura kina matumizi ya nyumbani tu basi bora liende..........
Napenda kuwapongeza wale waandikishaji wa vitambulisho vilivyopita vya Analojia walikuwa na uweledi mkubwa waliweza kuandika (handwriting) na kutoa picha kwa ukubwa unaostahili kuliko hawa wa kidigitali wanaofanya kazi katika kipindi hiki ambao wengine walikuwa hawajahi kukutana na Kompyuta lakini kwa maelekezo na mafunzo ya saa moja tu wanaingia kwenye zoezi kubwa kama hili.
Hivi tatizo ni nini? .................. Au ni wivu unanisumbua!!... naomba niishie hapo niachie wadau kuchangia kwa mustakabali mzuri wa nchi yetu.
↧
LOWASA ACHUKUWA FOMU YA URAISI CHADEMA
↧
MUONEKANO WA ENEO LA KITUNDA
↧